Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Isa akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, |
| 2 |
| “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. |
| 3 |
| Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja. |
| 4 |
| “Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’ |
| 5 |
| “Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. |
| 6 |
| Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua. |
| 7 |
| Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto. |
| 8 |
| “Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. |
| 9 |
| Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ |
| 10 |
| Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni. |
| 11 |
| “Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi. |
| 12 |
| Mfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. |
| 13 |
| “Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ |
| 14 |
| “Kwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.” |
| 15 |
| Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Isa katika maneno yake. |
| 16 |
| Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo. |
| 17 |
| Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?” |
| 18 |
| Lakini Isa, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? |
| 19 |
| Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari. |
| 20 |
| Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?” |
| 21 |
| Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Isa akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.” |
| 22 |
| Waliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao. |
| 23 |
| Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza swali, wakisema, |
| 24 |
| “Mwalimu, Musa alisema, ‘Kama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’ |
| 25 |
| Basi palikuwa na ndugu saba miongoni mwetu. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa, na kwa kuwa hakuwa na watoto, akamwachia nduguye yule mjane. |
| 26 |
| Ikatokea vivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili, na wa tatu, hadi wote saba. |
| 27 |
| Hatimaye, yule mwanamke naye akafa. |
| 28 |
| Sasa basi, siku ya ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba, kwa kuwa wote walikuwa wamemwoa huyo mwanamke?” |
| 29 |
| Isa akawajibu, “Mwapotoka kwa sababu hamjui Maandiko wala uweza wa Mungu. |
| 30 |
| Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. |
| 31 |
| Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma kile Mungu alichowaambia, kwamba, |
| 32 |
| ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.” |
| 33 |
| Ule umati wa watu uliposikia hayo, ulishangaa sana kwa mafundisho yake. |
| 34 |
| Mafarisayo waliposikia kwamba Isa alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja. |
| 35 |
| Mmoja wao, mtaalamu wa Torati, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema, |
| 36 |
| “Mwalimu, ni amri ipi katika Torati iliyo kuu kuliko zote?” |
| 37 |
| Isa akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ |
| 38 |
| Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. |
| 39 |
| Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ |
| 40 |
| Amri hizi mbili ndizo msingi wa Torati na Manabii.” |
| 41 |
| Wakati Mafarisayo walikuwa wamekusanyika pamoja, Isa akawauliza, |
| 42 |
| “Mnaonaje kuhusu Al-Masihi? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni Mwana wa Daudi. ” |
| 43 |
| Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Al-Masihi ‘Bwana’? Kwa maana asema, |
| 44 |
| “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” ’ |
| 45 |
| Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?” |
| 46 |
| Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Isa neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/matthew/022.mp3
28
22