|
| 1 |
|
| Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake, |
|
| 2 |
|
| wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa. |
|
| 3 |
|
| Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; |
|
| 4 |
|
| tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba. |
|
| 5 |
|
| Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? |
|
| 6 |
|
| Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; |
|
| 7 |
|
| Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, |
|
| 8 |
|
| Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. |
|
| 9 |
|
| Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. |
|
| 10 |
|
| Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. |
|
| 11 |
|
| Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; |
|
| 12 |
|
| wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; |
|
| 13 |
|
| huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo. |
|
| 14 |
|
| Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. |
|
| 15 |
|
| Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. |
|
| 16 |
|
| Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.] |
|
| 17 |
|
| Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano. |
|
| 18 |
|
| Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; |
|
| 19 |
|
| kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. |
|
| 20 |
|
| Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. |
|
| 21 |
|
| Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, |
|
| 22 |
|
| wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. |
|
| 23 |
|
| Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. |
|
| 24 |
|
| Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika. |
|
| 25 |
|
| Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake. |
|
| 26 |
|
| Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake. |
|
| 27 |
|
| Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. |
|
| 28 |
|
| Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto. |
|
| 29 |
|
| Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. |
|
| 30 |
|
| Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka. |
|
| 31 |
|
| Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. |
|
| 32 |
|
| Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. |
|
| 33 |
|
| Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, |
|
| 34 |
|
| akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. |
|
| 35 |
|
| Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. |
|
| 36 |
|
| Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari; |
|
| 37 |
|
| wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme. |
|
|
|
|