Maandiko Matakatifu 2018
|
| 1 |
| Mafarisayo na baadhi ya walimu wa Torati waliokuwa wametoka Yerusalemu wakakusanyika mbele ya Isa. |
| 2 |
| Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani, bila kunawa kama ilivyotakiwa na Torati ya dini ya Wayahudi. |
| 3 |
| Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata desturi za wazee wao. |
| 4 |
| Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba. |
| 5 |
| Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa Torati wakamuuliza Isa, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee, na badala yake wanakula kwa mikono najisi?” |
| 6 |
| Isa akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa: “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. |
| 7 |
| Huniabudu bure, nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’ |
| 8 |
| Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.” |
| 9 |
| Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu! |
| 10 |
| Kwa mfano, Musa alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ |
| 11 |
| Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu), |
| 12 |
| basi hawajibiki tena kumsaidia baba yake au mama yake. |
| 13 |
| Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya aina hiyo.” |
| 14 |
| Isa akaita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni, kila mmoja wenu na mwelewe jambo hili. |
| 15 |
| Hakuna kitu kinachomwingia mtu kimtiacho unajisi, lakini kile kimtokacho ndicho kimtiacho unajisi. [ |
| 16 |
| Kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia na asikie.]” |
| 17 |
| Akiisha kuuacha ule umati wa watu na kuingia ndani, wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano ule. |
| 18 |
| Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi? |
| 19 |
| Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Isa alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni “safi.”) |
| 20 |
| Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. |
| 21 |
| Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, |
| 22 |
| tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. |
| 23 |
| Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.” |
| 24 |
| Ndipo Isa akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha. |
| 25 |
| Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake. |
| 26 |
| Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria. Akamsihi Isa amtoe binti yake huyo pepo mchafu. |
| 27 |
| Isa akamwambia, “Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” |
| 28 |
| Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.” |
| 29 |
| Ndipo Isa akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, nenda zako nyumbani; yule pepo mchafu amemtoka binti yako.” |
| 30 |
| Akaenda zake nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, yule pepo mchafu akiwa amemtoka. |
| 31 |
| Kisha Isa akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli. |
| 32 |
| Huko, watu wakamletea Isa mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu na amponye. |
| 33 |
| Baadaye Isa akampeleka yule kiziwi kando mbali na watu, Isa akatia vidole vyake masikioni mwa yule mtu. Kisha akatema mate na kuugusa ulimi wa yule mtu. |
| 34 |
| Ndipo Isa akatazama mbinguni, akavuta hewa ndani kwa nguvu akamwambia, “Efatha!” Yaani, “Funguka!” |
| 35 |
| Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukaachiliwa, akaanza kuongea sawasawa. |
| 36 |
| Isa akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hizi. Lakini kadiri alivyowazuia, ndivyo walivyozidi kutangaza kwa bidii. |
| 37 |
| Walistaajabu mno. Wakasema, “Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!” |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahilinmm/mark/007.mp3
16
7