Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. |
| 2 |
| Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. |
| 3 |
| Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. |
| 4 |
| Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. |
| 5 |
| Maana hata nduguze hawakumwamini. |
| 6 |
| Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. |
| 7 |
| Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. |
| 8 |
| Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. |
| 9 |
| Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya. |
| 10 |
| Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. |
| 11 |
| Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule? |
| 12 |
| Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano. |
| 13 |
| Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. |
| 14 |
| Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha. |
| 15 |
| Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? |
| 16 |
| Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. |
| 17 |
| Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. |
| 18 |
| Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu. |
| 19 |
| Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? |
| 20 |
| Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? |
| 21 |
| Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia. |
| 22 |
| Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. |
| 23 |
| Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? |
| 24 |
| Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. |
| 25 |
| Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? |
| 26 |
| Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? |
| 27 |
| Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. |
| 28 |
| Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. |
| 29 |
| Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. |
| 30 |
| Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. |
| 31 |
| Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? |
| 32 |
| Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate. |
| 33 |
| Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. |
| 34 |
| Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. |
| 35 |
| Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? |
| 36 |
| Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja? |
| 37 |
| Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. |
| 38 |
| Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. |
| 39 |
| Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa. |
| 40 |
| Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule. |
| 41 |
| Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya? |
| 42 |
| Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi? |
| 43 |
| Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake. |
| 44 |
| Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika. |
| 45 |
| Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? |
| 46 |
| Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. |
| 47 |
| Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? |
| 48 |
| Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? |
| 49 |
| Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. |
| 50 |
| Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), |
| 51 |
| Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? |
| 52 |
| Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/john/007.mp3
21
7