|
| 1 |
|
| Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana Isa lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu. |
|
| 2 |
|
| Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini. |
|
| 3 |
|
| Lakini Bwana Isa ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu. |
|
| 4 |
|
| Nasi tuna tumaini katika Bwana Isa ya kuwa mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. |
|
| 5 |
|
| Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mwenyezi Mungu na katika saburi ya Al-Masihi. |
|
| 6 |
|
| Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Isa Al-Masihi, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. |
|
| 7 |
|
| Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, |
|
| 8 |
|
| wala hatukula chakula cha mtu yeyote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote miongoni mwenu. |
|
| 9 |
|
| Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe kielelezo. |
|
| 10 |
|
| Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.” |
|
| 11 |
|
| Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. |
|
| 12 |
|
| Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Isa Al-Masihi, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe. |
|
| 13 |
|
| Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema. |
|
| 14 |
|
| Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu. |
|
| 15 |
|
| Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. |
|
| 16 |
|
| Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote. |
|
| 17 |
|
| Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo. |
|
| 18 |
|
| Neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi nyote. Amen. |
|
|
|
|