Kiswahili Biblia 2005
|
| 1 |
| Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. |
| 2 |
| Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba. |
| 3 |
| Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu. |
| 4 |
| Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; |
| 5 |
| wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. |
| 6 |
| Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. |
| 7 |
| Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. |
| 8 |
| Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. |
| 9 |
| Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki. |
| 10 |
| Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. |
| 11 |
| Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. |
| 12 |
| Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. |
| 13 |
| Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. |
| 14 |
| Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. |
| 15 |
| Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. |
| 16 |
| Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. |
| 17 |
| Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. |
| 18 |
| Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile. |
| 19 |
| Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; |
| 20 |
| ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. |
| 21 |
| Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana. |
| 22 |
| Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake. |
|
| Hifadhi Vidokezo |
https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/1samuel/008.mp3
31
8