× Lugha Ulaya Kirusi Kibelarusi Kiukreni Kipolishi Kisabia Kibulgaria Kislovakia Kicheki Kiromania Kimongolia Azerbaijan Kiarmenia Kijojiajia Kialbania Avar Bashkir Kitatari Chechen Kislovenia Kikroeshia Kiestonia Kilatvia Kilithuania Kihungari Kifini Kinorwe Kiswidi Kiaislandi Kigiriki Kimasedonia Kijerumani Bavaria Kiholanzi Kidenmaki Kiwelisi Gaelic Kiayalandi Kifaransa Kibasque Kikatalani Kiitaliano Galacian Romani Bosnian Marekani Kaskazini Kiingereza Amerika Kusini Kihispania Kireno Kiguarani Quechuan Aymara Amerika ya Kati Jamaican Nahuatl Kiche Q'eqchi Kihaiti Asia ya Mashariki Kichina Kijapani Kikorea Kimongolia Uyghur Hmong Asia ya Kusini Mashariki Malaysia Kiburma Hakha Chin Kinepali Cebuano Tagalog Kambodia Thai Kiindonesia Kivietinamu Kijava Lao Iban Iu Mien Kachin Lahu Aceh Balinese Bugis Pampanga Sasak Shan Waray Asia ya Kusini Kihindi Оdia Awadhi Mizo Kannada Kimalayalam Marathi Kigujarati Kitamil Kitelugu Kipunjabi Kurukh Kiassam Maithili Kibangali Kiurdu Sinhala Dogri Haryanvi Meitei Konkani Santali Kisindhi Koya Thado Sanskrit Devanagari Adilabad Gondi Ahirani Balochi Bundeli Chhattisgarhi Garhwali Kangri Kumaoni Mewari Munda Sadri Seraiki Shekhawati Sylheti Asia ya Kati Kikirigizi Kiuzbeki Tajik Waturuki Kazakhstan Karakalpak Mashariki ya Kati Kituruki Kiebrania Kiarabu Kiajemi Kikurdi Kipashto Kikatili Afrika Kiafrika Kixhosa Kizulu Ndebele Kisotho Kiamhari Wolaytta Nigeria Mossi Ika Dinka Kabyle Ewe Kiswahili Morocco Kisalia Kiingereza Madagascar Igbo Lingala Baoule Siswati Kitsonga Tswana Gambia Kiyoruba Kamba Kinyarwanda Kihausa Chewa Kiluo Makua Dyula Fulfulde Kalenjin Kikikuyu Kikwango Kirundi Krio Nigerian Pidgin Oromo Tshiluba Tshivenda Twi Umbundu Lugbara Luguru Pular Gussi Mmasai Turkana Moba Nuer Shilluk Tamasheq Makonde Bemba Fon Hadiyya Ibibio Kimbundu Kimiiru Lango Liberian Kreyol Lomwe Mende Morisyen Ndau Nyankole Sena Sidamo Soga Songe Sukuma Tarifit Teso Tiv Zande Dagbani Bara la Australia New Zealand Papua Mpya Guinea Lugha za Zamani Aramaic Kilatini Kiesperanto 1 1 1 SRUV 1997 NMM 2018TKU 2017NEN 2015RSUVDC 2013SWC 2002BHN 2001SCLDC10 2001SRUV 1997SUV 1997BHNTLK 1993SRB 1937SWZZB192118501 1 1 Yohane MwanzoKutokaWalawiHesabuKumbukumbu la SheriaYoshuaWaamuziRuthu1 Samueli2 Samueli1 Wafalme2 Wafalme1 Mambo ya Nyakati2 Mambo ya NyakatiEzraNehemiaEstaYobuZaburiMethaliMhubiriHekimaIsayaYeremiaMaombolezoEzekieliDanieliHoseaYoeliAmosiObadiaYonaMikaNahumuHabakukiSefaniaHagaiZekariaMalaki--- --- ---MatthayoMarkoLukaYohaneWaromaMatendo ya Mitume1 Wakorinto2 WakorintoWagalatiaWaefesoWafilipiWakolosai1 Wathesalonike2 Wathesalonike1 Timotheo2 TimotheoTitoFilemoniWaebraniaYakobo1 Petro2 Petro1 Yohane2 Yohane3 YohaneYudaUfunuo wa Yohane1 1 1 1 1234567891011121314151617181920211 1 1 : 1 1234567891011121314151617181920212223242526272829303132333435363738394041424344454647484950511 1 1 Kiswahili Biblia 1997 Yohane 1 Hifadhi Vidokezo 1Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.2Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.3Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.4Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.5Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.6Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.7Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.8Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.9Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.10Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.11Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.12Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;13waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.14Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.15Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.16Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.17Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.18Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.19Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?20Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.21Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.22Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?23Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.24Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.25Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?26Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.27Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.28Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.29Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!30Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.31Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.32Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.33Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.34Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.35Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.36Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!37Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.38Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?39Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.40Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.41Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).42Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).43Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.44Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro.45Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.46Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.47Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.48Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.49Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli.50Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya.51Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.Swahili Bible 1997 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved. Kiswahili Biblia 1997 Yohane 1 00:00:00 00:00:00 0.5x 2.0x https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/john/001.mp3 21 1