× Lugha Ulaya Kirusi Kibelarusi Kiukreni Kipolishi Kisabia Kibulgaria Kislovakia Kicheki Kiromania Kimongolia Azerbaijan Kiarmenia Kijojiajia Kialbania Avar Bashkir Kitatari Chechen Kislovenia Kikroeshia Kiestonia Kilatvia Kilithuania Kihungari Kifini Kinorwe Kiswidi Kiaislandi Kigiriki Kimasedonia Kijerumani Bavaria Kiholanzi Kidenmaki Kiwelisi Gaelic Kiayalandi Kifaransa Kibasque Kikatalani Kiitaliano Galacian Romani Bosnian Marekani Kaskazini Kiingereza Amerika Kusini Kihispania Kireno Kiguarani Quechuan Aymara Amerika ya Kati Jamaican Nahuatl Kiche Q'eqchi Kihaiti Asia ya Mashariki Kichina Kijapani Kikorea Kimongolia Uyghur Hmong Asia ya Kusini Mashariki Malaysia Kiburma Hakha Chin Kinepali Cebuano Tagalog Kambodia Thai Kiindonesia Kivietinamu Kijava Lao Iban Iu Mien Kachin Lahu Aceh Balinese Bugis Pampanga Sasak Shan Waray Asia ya Kusini Kihindi Оdia Awadhi Mizo Kannada Kimalayalam Marathi Kigujarati Kitamil Kitelugu Kipunjabi Kurukh Kiassam Maithili Kibangali Kiurdu Sinhala Dogri Haryanvi Meitei Konkani Santali Kisindhi Koya Thado Sanskrit Devanagari Adilabad Gondi Ahirani Balochi Bundeli Chhattisgarhi Garhwali Kangri Kumaoni Mewari Munda Sadri Seraiki Shekhawati Sylheti Asia ya Kati Kikirigizi Kiuzbeki Tajik Waturuki Kazakhstan Karakalpak Mashariki ya Kati Kituruki Kiebrania Kiarabu Kiajemi Kikurdi Kipashto Kikatili Afrika Kiafrika Kixhosa Kizulu Ndebele Kisotho Kiamhari Wolaytta Nigeria Mossi Ika Dinka Kabyle Ewe Kiswahili Morocco Kisalia Kiingereza Madagascar Igbo Lingala Baoule Siswati Kitsonga Tswana Gambia Kiyoruba Kamba Kinyarwanda Kihausa Chewa Kiluo Makua Dyula Fulfulde Kalenjin Kikikuyu Kikwango Kirundi Krio Nigerian Pidgin Oromo Tshiluba Tshivenda Twi Umbundu Lugbara Luguru Pular Gussi Mmasai Turkana Moba Nuer Shilluk Tamasheq Makonde Bemba Fon Hadiyya Ibibio Kimbundu Kimiiru Lango Liberian Kreyol Lomwe Mende Morisyen Ndau Nyankole Sena Sidamo Soga Songe Sukuma Tarifit Teso Tiv Zande Bara la Australia New Zealand Papua Mpya Guinea Lugha za Zamani Aramaic Kilatini Kiesperanto 1 1 1 SRUV 1997 NMM 2018TKU 2017NEN 2015RSUVDC 2013SWC 2002BHN 2001SCLDC10 2001SRUV 1997SUV 1997BHNTLK 1993SRB 1937SWZZB192118501 1 1 Waefeso MwanzoKutokaWalawiHesabuKumbukumbu la SheriaYoshuaWaamuziRuthu1 Samueli2 Samueli1 Wafalme2 Wafalme1 Mambo ya Nyakati2 Mambo ya NyakatiEzraNehemiaEstaYobuZaburiMethaliMhubiriHekimaIsayaYeremiaMaombolezoEzekieliDanieliHoseaYoeliAmosiObadiaYonaMikaNahumuHabakukiSefaniaHagaiZekariaMalaki--- --- ---MatthayoMarkoLukaYohaneWaromaMatendo ya Mitume1 Wakorinto2 WakorintoWagalatiaWaefesoWafilipiWakolosai1 Wathesalonike2 Wathesalonike1 Timotheo2 TimotheoTitoFilemoniWaebraniaYakobo1 Petro2 Petro1 Yohane2 Yohane3 YohaneYudaUfunuo wa Yohane1 1 1 4 1234561 1 1 : 1 12345678910111213141516171819202122232425262728293031321 1 1 Kiswahili Biblia 1997 Waefeso 4 Hifadhi Vidokezo 1Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;2kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;3na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.4Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.5Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.6Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.7Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.8Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.9Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?10Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.11Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;12kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;13hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;14ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.15Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.16Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.17Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao;18ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;19ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.20Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo;21ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu,22mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;23na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;24mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.25Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.26Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;27wala msimpe Ibilisi nafasi.28Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.29Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.30Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.31Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;32tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.Swahili Bible 1997 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved. Kiswahili Biblia 1997 Waefeso 4 00:00:00 00:00:00 0.5x 2.0x https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/ephesians/004.mp3 6 4