× Lugha Ulaya Kirusi Kibelarusi Kiukreni Kipolishi Kisabia Kibulgaria Kislovakia Kicheki Kiromania Kimongolia Azerbaijan Kiarmenia Kijojiajia Kialbania Avar Bashkir Kitatari Chechen Kislovenia Kikroeshia Kiestonia Kilatvia Kilithuania Kihungari Kifini Kinorwe Kiswidi Kiaislandi Kigiriki Kimasedonia Kijerumani Bavaria Kiholanzi Kidenmaki Kiwelisi Gaelic Kiayalandi Kifaransa Kibasque Kikatalani Kiitaliano Galacian Romani Bosnian Marekani Kaskazini Kiingereza Amerika Kusini Kihispania Kireno Kiguarani Quechuan Aymara Amerika ya Kati Jamaican Nahuatl Kiche Q'eqchi Kihaiti Asia ya Mashariki Kichina Kijapani Kikorea Kimongolia Uyghur Hmong Asia ya Kusini Mashariki Malaysia Kiburma Hakha Chin Kinepali Cebuano Tagalog Kambodia Thai Kiindonesia Kivietinamu Kijava Lao Iban Iu Mien Kachin Lahu Aceh Balinese Bugis Pampanga Sasak Shan Waray Asia ya Kusini Kihindi Оdia Awadhi Mizo Kannada Kimalayalam Marathi Kigujarati Kitamil Kitelugu Kipunjabi Kurukh Kiassam Maithili Kibangali Kiurdu Sinhala Dogri Haryanvi Meitei Konkani Santali Kisindhi Koya Thado Sanskrit Devanagari Adilabad Gondi Ahirani Balochi Bundeli Chhattisgarhi Garhwali Kangri Kumaoni Mewari Munda Sadri Seraiki Shekhawati Sylheti Asia ya Kati Kikirigizi Kiuzbeki Tajik Waturuki Kazakhstan Karakalpak Mashariki ya Kati Kituruki Kiebrania Kiarabu Kiajemi Kikurdi Kipashto Kikatili Afrika Kiafrika Kixhosa Kizulu Ndebele Kisotho Kiamhari Wolaytta Nigeria Mossi Ika Dinka Kabyle Ewe Kiswahili Morocco Kisalia Kiingereza Madagascar Igbo Lingala Baoule Siswati Kitsonga Tswana Gambia Kiyoruba Kamba Kinyarwanda Kihausa Chewa Kiluo Makua Dyula Fulfulde Kalenjin Kikikuyu Kikwango Kirundi Krio Nigerian Pidgin Oromo Tshiluba Tshivenda Twi Umbundu Lugbara Luguru Pular Gussi Mmasai Turkana Moba Nuer Shilluk Tamasheq Makonde Bemba Fon Hadiyya Ibibio Kimbundu Kimiiru Lango Liberian Kreyol Lomwe Mende Morisyen Ndau Nyankole Sena Sidamo Soga Songe Sukuma Tarifit Teso Tiv Zande Dagbani Bara la Australia New Zealand Papua Mpya Guinea Lugha za Zamani Aramaic Kilatini Kiesperanto 1 1 1 SRUV 1997 NMM 2018TKU 2017NEN 2015RSUVDC 2013SWC 2002BHN 2001SCLDC10 2001SRUV 1997SUV 1997BHNTLK 1993SRB 1937SWZZB192118501 1 1 1 Timotheo MwanzoKutokaWalawiHesabuKumbukumbu la SheriaYoshuaWaamuziRuthu1 Samueli2 Samueli1 Wafalme2 Wafalme1 Mambo ya Nyakati2 Mambo ya NyakatiEzraNehemiaEstaYobuZaburiMethaliMhubiriHekimaIsayaYeremiaMaombolezoEzekieliDanieliHoseaYoeliAmosiObadiaYonaMikaNahumuHabakukiSefaniaHagaiZekariaMalaki--- --- ---MatthayoMarkoLukaYohaneWaromaMatendo ya Mitume1 Wakorinto2 WakorintoWagalatiaWaefesoWafilipiWakolosai1 Wathesalonike2 Wathesalonike1 Timotheo2 TimotheoTitoFilemoniWaebraniaYakobo1 Petro2 Petro1 Yohane2 Yohane3 YohaneYudaUfunuo wa Yohane1 1 1 1 1234561 1 1 : 1 12345678910111213141516171819201 1 1 Kiswahili Biblia 1997 1 Timotheo 1 Hifadhi Vidokezo 1Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, taraja letu;2kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.3Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;4wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo.5Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.6Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili;7wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.8Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;9akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,10na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;11kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.12Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;13ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.14Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.15Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.16Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.17Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.18Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri;19uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.20Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.Swahili Bible 1997 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved. Kiswahili Biblia 1997 1 Timotheo 1 00:00:00 00:00:00 0.5x 2.0x https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/1timothy/001.mp3 6 1