× Lugha Ulaya Kirusi Kibelarusi Kiukreni Kipolishi Kisabia Kibulgaria Kislovakia Kicheki Kiromania Kimongolia Azerbaijan Kiarmenia Kijojiajia Kialbania Avar Bashkir Kitatari Chechen Kislovenia Kikroeshia Kiestonia Kilatvia Kilithuania Kihungari Kifini Kinorwe Kiswidi Kiaislandi Kigiriki Kimasedonia Kijerumani Bavaria Kiholanzi Kidenmaki Kiwelisi Gaelic Kiayalandi Kifaransa Kibasque Kikatalani Kiitaliano Galacian Romani Bosnian Marekani Kaskazini Kiingereza Amerika Kusini Kihispania Kireno Kiguarani Quechuan Aymara Amerika ya Kati Jamaican Nahuatl Kiche Q'eqchi Kihaiti Asia ya Mashariki Kichina Kijapani Kikorea Kimongolia Uyghur Hmong Asia ya Kusini Mashariki Malaysia Kiburma Hakha Chin Kinepali Cebuano Tagalog Kambodia Thai Kiindonesia Kivietinamu Kijava Lao Iban Iu Mien Kachin Lahu Aceh Balinese Bugis Pampanga Sasak Shan Waray Asia ya Kusini Kihindi Оdia Awadhi Mizo Kannada Kimalayalam Marathi Kigujarati Kitamil Kitelugu Kipunjabi Kurukh Kiassam Maithili Kibangali Kiurdu Sinhala Dogri Haryanvi Meitei Konkani Santali Kisindhi Koya Thado Sanskrit Devanagari Adilabad Gondi Ahirani Balochi Bundeli Chhattisgarhi Garhwali Kangri Kumaoni Mewari Munda Sadri Seraiki Shekhawati Sylheti Asia ya Kati Kikirigizi Kiuzbeki Tajik Waturuki Kazakhstan Karakalpak Mashariki ya Kati Kituruki Kiebrania Kiarabu Kiajemi Kikurdi Kipashto Kikatili Afrika Kiafrika Kixhosa Kizulu Ndebele Kisotho Kiamhari Wolaytta Nigeria Mossi Ika Dinka Kabyle Ewe Kiswahili Morocco Kisalia Kiingereza Madagascar Igbo Lingala Baoule Siswati Kitsonga Tswana Gambia Kiyoruba Kamba Kinyarwanda Kihausa Chewa Kiluo Makua Dyula Fulfulde Kalenjin Kikikuyu Kikwango Kirundi Krio Nigerian Pidgin Oromo Tshiluba Tshivenda Twi Umbundu Lugbara Luguru Pular Gussi Mmasai Turkana Moba Nuer Shilluk Tamasheq Makonde Bemba Fon Hadiyya Ibibio Kimbundu Kimiiru Lango Liberian Kreyol Lomwe Mende Morisyen Ndau Nyankole Sena Sidamo Soga Songe Sukuma Tarifit Teso Tiv Zande Dagbani Bara la Australia New Zealand Papua Mpya Guinea Lugha za Zamani Aramaic Kilatini Kiesperanto 1 1 1 SRUV 1997 NMM 2018TKU 2017NEN 2015RSUVDC 2013SWC 2002BHN 2001SCLDC10 2001SRUV 1997SUV 1997BHNTLK 1993SRB 1937SWZZB192118501 1 1 Waebrania MwanzoKutokaWalawiHesabuKumbukumbu la SheriaYoshuaWaamuziRuthu1 Samueli2 Samueli1 Wafalme2 Wafalme1 Mambo ya Nyakati2 Mambo ya NyakatiEzraNehemiaEstaYobuZaburiMethaliMhubiriHekimaIsayaYeremiaMaombolezoEzekieliDanieliHoseaYoeliAmosiObadiaYonaMikaNahumuHabakukiSefaniaHagaiZekariaMalaki--- --- ---MatthayoMarkoLukaYohaneWaromaMatendo ya Mitume1 Wakorinto2 WakorintoWagalatiaWaefesoWafilipiWakolosai1 Wathesalonike2 Wathesalonike1 Timotheo2 TimotheoTitoFilemoniWaebraniaYakobo1 Petro2 Petro1 Yohane2 Yohane3 YohaneYudaUfunuo wa Yohane1 1 1 12 123456789101112131 1 1 : 1 12345678910111213141516171819202122232425262728291 1 1 Kiswahili Biblia 1997 Waebrania 12 Hifadhi Vidokezo 1Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,2tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.3Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.4Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;5tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;6Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.7Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?8Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.9Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?10Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.11Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.12Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,13mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.14Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;15mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.16Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.17Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.18Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,19na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine;20maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe.21Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.22Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,23mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,24na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.25Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;26ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.27Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.28Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;29maana Mungu wetu ni moto ulao.Swahili Bible 1997 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved. Kiswahili Biblia 1997 Waebrania 12 00:00:00 00:00:00 0.5x 2.0x https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/hebrews/012.mp3 13 12