× Lugha Ulaya Kirusi Kibelarusi Kiukreni Kipolishi Kisabia Kibulgaria Kislovakia Kicheki Kiromania Kimongolia Azerbaijan Kiarmenia Kijojiajia Kialbania Avar Bashkir Kitatari Chechen Kislovenia Kikroeshia Kiestonia Kilatvia Kilithuania Kihungari Kifini Kinorwe Kiswidi Kiaislandi Kigiriki Kimasedonia Kijerumani Bavaria Kiholanzi Kidenmaki Kiwelisi Gaelic Kiayalandi Kifaransa Kibasque Kikatalani Kiitaliano Galacian Romani Bosnian Marekani Kaskazini Kiingereza Amerika Kusini Kihispania Kireno Kiguarani Quechuan Aymara Amerika ya Kati Jamaican Nahuatl Kiche Q'eqchi Kihaiti Asia ya Mashariki Kichina Kijapani Kikorea Kimongolia Uyghur Hmong Asia ya Kusini Mashariki Malaysia Kiburma Hakha Chin Kinepali Cebuano Tagalog Kambodia Thai Kiindonesia Kivietinamu Kijava Lao Iban Iu Mien Kachin Lahu Aceh Balinese Bugis Pampanga Sasak Shan Waray Asia ya Kusini Kihindi Оdia Awadhi Mizo Kannada Kimalayalam Marathi Kigujarati Kitamil Kitelugu Kipunjabi Kurukh Kiassam Maithili Kibangali Kiurdu Sinhala Dogri Haryanvi Meitei Konkani Santali Kisindhi Koya Thado Sanskrit Devanagari Adilabad Gondi Ahirani Balochi Bundeli Chhattisgarhi Garhwali Kangri Kumaoni Mewari Munda Sadri Seraiki Shekhawati Sylheti Asia ya Kati Kikirigizi Kiuzbeki Tajik Waturuki Kazakhstan Karakalpak Mashariki ya Kati Kituruki Kiebrania Kiarabu Kiajemi Kikurdi Kipashto Kikatili Afrika Kiafrika Kixhosa Kizulu Ndebele Kisotho Kiamhari Wolaytta Nigeria Mossi Ika Dinka Kabyle Ewe Kiswahili Morocco Kisalia Kiingereza Madagascar Igbo Lingala Baoule Siswati Kitsonga Tswana Gambia Kiyoruba Kamba Kinyarwanda Kihausa Chewa Kiluo Makua Dyula Fulfulde Kalenjin Kikikuyu Kikwango Kirundi Krio Nigerian Pidgin Oromo Tshiluba Tshivenda Twi Umbundu Lugbara Luguru Pular Gussi Mmasai Turkana Moba Nuer Shilluk Tamasheq Makonde Bemba Fon Hadiyya Ibibio Kimbundu Kimiiru Lango Liberian Kreyol Lomwe Mende Morisyen Ndau Nyankole Sena Sidamo Soga Songe Sukuma Tarifit Teso Tiv Zande Dagbani Bara la Australia New Zealand Papua Mpya Guinea Lugha za Zamani Aramaic Kilatini Kiesperanto 1 1 1 SRUV 1997 NMM 2018TKU 2017NEN 2015RSUVDC 2013SWC 2002BHN 2001SCLDC10 2001SRUV 1997SUV 1997BHNTLK 1993SRB 1937SWZZB192118501 1 1 Ufunuo wa Yohane MwanzoKutokaWalawiHesabuKumbukumbu la SheriaYoshuaWaamuziRuthu1 Samueli2 Samueli1 Wafalme2 Wafalme1 Mambo ya Nyakati2 Mambo ya NyakatiEzraNehemiaEstaYobuZaburiMethaliMhubiriHekimaIsayaYeremiaMaombolezoEzekieliDanieliHoseaYoeliAmosiObadiaYonaMikaNahumuHabakukiSefaniaHagaiZekariaMalaki--- --- ---MatthayoMarkoLukaYohaneWaromaMatendo ya Mitume1 Wakorinto2 WakorintoWagalatiaWaefesoWafilipiWakolosai1 Wathesalonike2 Wathesalonike1 Timotheo2 TimotheoTitoFilemoniWaebraniaYakobo1 Petro2 Petro1 Yohane2 Yohane3 YohaneYudaUfunuo wa Yohane1 1 1 1 123456789101112131415161718192021221 1 1 : 1 12345678910111213141516171819201 1 1 Kiswahili Biblia 1997 Ufunuo wa Yohane 1 Hifadhi Vidokezo 1Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;2aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.3Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.4Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;5tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,6na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.7Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.8Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.9Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.10Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,11ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.12Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;13na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.14Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;15na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.16Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.17Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,18na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.19Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.20Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.Swahili Bible 1997 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved. Kiswahili Biblia 1997 Ufunuo wa Yohane 1 00:00:00 00:00:00 0.5x 2.0x https://beblia.bible:81/BibleAudio/swahili/revelation/001.mp3 22 1