Toleo la Bibilia Linganisha
- |
|---|
| 1 |
| Yesu akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. |
| 2 |
| Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda. Yesu alipoona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu, dhambi zako zimesamehewa.” |
| 3 |
| Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa sheria wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” |
| Swahili Bible 2025
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc |
| 1 |
| Isa akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. |
| 2 |
| Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa.” |
| 3 |
| Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” |
| Swahili Bible 2024
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc |
| 1 |
| Isa akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. |
| 2 |
| Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa.” |
| 3 |
| Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” |
| Swahili Bible 2018
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™ Hakimiliki © 2018 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Scriptures™ |
| 1 |
| Yesu akapanda katika mashua na akasafiri kwa kukatisha ziwa kurudi kwenye mji wake. |
| 2 |
| Baadhi ya watu wakamletea mtu aliyepooza akiwa amelala kwenye machela. Yesu alipoona imani waliyokuwa nayo, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Changamka mtoto wangu! Dhambi zako zimesamehewa.” |
| 3 |
| Baadhi ya walimu wa sheria walisikia alichosema Yesu. Wakaambizana wao kwa wao, “Si anamtukana Mungu mtu huyu akasema hivyo!” |
| Swahili Bible 2017
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi Toleo la Awali © 2017 Bible League International |
| 1 |
| Akapanda katika mashua, akavuka, akafika mjini kwao. |
| 2 |
| Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, akiwa amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. |
| 3 |
| Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. |
| Swahili Bible 2013
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013 |
| 1 |
| Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. |
| 2 |
| Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. |
| 3 |
| Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. |
| Swahili Bible 2005
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005 |
| 1 |
| Yesu akaingia katika chombo akavuka tena ziwa kwenda upande wa magaribi, naye akafika katika muji wake. |
| 2 |
| Na kule wakamuletea mutu mwenye ugonjwa wa kupooza, akilala juu ya kipoyi. Yesu alipoona namna watu wale walivyomwaminia, akamwambia yule mwenye kupooza: “Mutoto wangu, ujipe moyo! Zambi zako zimesamehewa!” |
| 3 |
| Halafu walimu wamoja wa Sheria waliokuwa pale wakajisemesha: “Mutu huyu anamutukana Mungu!” |
| Swahili Bible 2002
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002 |
| 1 |
| Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake. |
| 2 |
| Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.” |
| 3 |
| Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” |
| Swahili Bible 2001
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki - 1995, 2001 |
| 1 |
| Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake. |
| 2 |
| Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.” |
| 3 |
| Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” |
| Swahili Bible 1995
Swahili Common Language DC Bible: Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki © Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya, 1995, 2001. Haki zote zimehifadhiwa |
| 1 |
| Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake. |
| 2 |
| Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.” |
| 3 |
| Baadhi ya waalimu wa sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” |
| Swahili Bible 1993
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993 |
| 1 |
| Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. |
| 2 |
| Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. |
| 3 |
| Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. |
| Swahili Bible 1952
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa. |
| 1 |
| *Akaingia chomboni, akavuka, akafika mjini mwake yeye. |
| 2 |
| Papo hapo wakamletea mgonjwa wa kupooza aliyelala kitandani. Yesu alipoona, walivyomtegemea, akamwambia mwenye kupooza: Tulia, mwanangu! Makosa yako yameondolea. |
| 3 |
| Ndipo, waandishi waliokuwako waliposema mioyoni: Huyu anambeza Mungu. |
| Swahili Bible 1937
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937 |
| 1 |
| AKAPANDA chomboni, akavuka, akafika mjini kwake. |
| 2 |
| Wakamletea mgonjwa wa kupooza, amelala kitandani: na Yesu, akiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa wa kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanaugu; umeondolewa dhambi zako. |
| 3 |
| Baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. |
| Swahili Bible 1921
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921 |
| 1 |
| Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake. |
| 2 |
| Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.” |
| 3 |
| Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu anamkufuru Mungu!” |
| Swahili Bible 1850
Portions of the New Testament in the Swahili Language of Kenya, Mozambique, Somalia, and Tanzania, translation by Dr. Johann Ludvig Krapf completed in 1850 |