Mistari ya Bibilia Kwenye Mada

Mada
Mungu
Tabia nzuri
Tabia Mbaya
Dhambi
Maisha
Kanisa
Siri
Malaika na Mapepo
Ishara za Math
Ziada
Mungu: [Baraka]
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”
Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.
Naye Mungu wangu atawajaza ninyi kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu.
Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.
[24] “ ‘ “BWANA akubariki na kukulinda; [25] BWANA akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili;
[6] Msijisumbue kwa jambo lo lote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. [7] Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itawalinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
[7] “Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika BWANA, ambaye matumaini yake ni katika BWANA. [8] Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji. Hauogopi wakati wa joto ujapo; majani yake ni mabichi daima. Hauna hofu katika mwaka wa ukame na hautaacha kuzaa matunda.”
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu na kukusaidia; nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.
[16] akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, [17] hakika, nitakubariki na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
[28] Mungu na akupe umande kutoka mbinguni na utajiri wa duniani: wingi wa nafaka na divai mpya. [29] Mataifa na yakutumikie na mataifa yakusujudie. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wakusujudie. Walaaniwe wale wakulaanio, nao wale wakubarikio wabarikiwe.”
[1] Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi au kuketi katika baraza la wenye mizaha. [2] Bali huifurahia sheria ya BWANA, naye huitafakari hiyo sheria mchana na usiku. [3] Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lo lote afanyalo hufanikiwa.
[1] (Zaburi Ya Daudi) BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. [2] Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, [3] huifanya upya nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. [4] Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.
[3] Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake nakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. [4] Namwita BWANA, yeye anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali aliyezaliwa na Mungu hujilinda wala yule mwovu hawezi kumdhuru.
Nijapopita katikati ya shida, wewe unayahifadhi maisha yangu, unanyosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itawalinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Swahili Bible 2025
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc